Friday, 18 December 2015

on Leave a Comment

Video:Bomoa Bomoa Dar es Salaam Disemba 17 Sio Mchezo!!


17 Dec 2015 kazi ya kuwahamisha wananchi wote waishiyo katika maeneo hatarishi iliendelea kwa kuzibomoa nyumba zote zilizopo mabondeni katika baadhi ya maeneo Dar es salaam ikiwa ni pamoja na bonde la Msimbazi lililopo Kinondoni, 

tazama hii video kujionea mwenyewe

Continue Reading here...
on Leave a Comment

Washitakiwa TRA Waachiwa kwa Dhamana


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es salaam yawaachia kwa dhamana ya shilingi bilioni 2 .1 washitakiwa 3 kati ya 8 wanaotuhumiwa kwa makosa ya hujuma katika ukusanyaji mapato TRA.

Continue Reading here...
on 1 comment

Serikali Yatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2016


Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza  mwakani  kutokana na matokeo ya darasa la saba  ambapo wanafunzi  427,60 kati ya  844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi  844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.

Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Lorraine Marriot Miss Universe Tanzania 2015 ndani ya Las Vegas na Vazi la Taifa


Lorraine Marriot (pichani) akiwa katika vazi la ubunifu la Taifa .Vazi hili limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar na imeitwa ‘Angel of Ivory’ maana inaonyesha Malaika wa Tanzania anayelinda Tembo wanaouwawa kwa ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu.

Huyu malaika wa Tanzania yupo kwa ajili ya kuwalinda Tembo na rasilimali zetu na kuwaadhibisha majangili. Nguo yake imeshonwa kwa ubunifu na umahiri mkubwa na hekaheka limebuniwa na Mwanakombo Salim. Pia kabeba fimbo la kimasai iliyonakshiwa na rangi za taifa.

Rangi nyekundu ni alama ya damu ya tembo iliyomwagika na kusafishwa na malaika huyu.


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Newspapers Headlines in Kenya 18 December





Continue Reading here...
on Leave a Comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 18











Continue Reading here...
on Leave a Comment

Tanzania:Vyombo vya Habari kuwalipa wasanii wanapopiga Nyimbo zao


Serikali ya awamu ya tano imeanza kutimiza kwa vitendo kauli ya kuifanya sanaa kuwa moja ya shughuli za kiuchumi baada ya kupitisha sheria ambayo inavitaka vyombo vya habari hapa nchini kuwalipa wanamuziki pindi wanapotumia nyimbo zao.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji CHARLES MWIJAGE amesema sheria hiyo itaanza kufanya kazi JANUARY MOJA mwaka 2016 huku waziri wa habari, utamaduni , sanaa na michezo NAPE NNAUYE akisema sasa wameanza kutekeleza yale waliyoyapanga kuyanfanya kwenye kukuza sanaa hapa nchini.

Katika kutimiza suala hilo chama cha hakimiliki hapa nchini (COSOTA) kimeingia mkataba na kampuni ya CMEA ili kuweza kufuatilia mapato ya kituo cha RADIO au TELEVISION inayopiga kazi ya mwanamuziki na kuweza kujua malipo yake yawe ya namna gani kwa mwezi.



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Spika wa Bunge Job Ndugai Yupo India kwa Matibabu.


Spika wa Bunge, Job Ndugai ni mgonjwa na yupo India kwa matibabu.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa Ndugai yuko nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake bila ya kusema amekwenda nchi gani wala ugonjwa unaomsumbua.

“Ni kweli Spika yupo nje, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi tu, siyo kwamba anaumwa sana, hapana ila hii ni mara ya pili kwenda kufanya uchunguzi huo. Hata ukitaka kuzungumza naye mpigie simu mtazungumza naye maana hali yake inaendelea vizuri na yuko salama,”alisema Dk Kashilila.

Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alipopigiwa simu ili kujua kama kiongozi huyo yuko huko, alisema:

“Ni kweli yuko hapa India kwa matibabu na anaendelea vizuri. Unaweza kumpigia wewe mwenyewe uzungumze naye.”

 Alisema Kijazi bila kuweka wazi kwamba yuko hospitali gani na nini hasa kinachomsumbua.


Continue Reading here...

Thursday, 17 December 2015

on Leave a Comment

Zitto Kabwe Aibuka na Kutetea Uteuzi wa Waziri Profesa Muhongo....Ashangaa Wanaoupinga


Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.

Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪TegetaEscrow. 

Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. 

Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?

 Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?

Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. 

Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO

2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo

By: Zitto Kabwe


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Serikali Yatoa Siku 14 Kwa Wageni Walioajiriwa Nchini Bila Kuwa na Vibali Halali


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Rais Magufuli HATANII Awafukuza Kazi Watumishi wanne wa Serikali Waliosafiri kwenda nje ya nchi bila Ruhusa


Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 17








Continue Reading here...