Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi
waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao
walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa
watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na
Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari
kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Agizo hilo la Rais Magufuli lilitolewa jana na Balozi Mkuu
Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa
atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.
0 comments:
Post a Comment