Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee
Ummy Mwalimu amepiga marufuku biashara ya uuzaji wa matunda
yaliyokatwakatwa pamoja na uuzaji wa chakula katika mazingira yasiyo
salama ili kukabiliana na ugonjwa wa KIPINDUPINDU ambao umesambaa katika mikoa
21 ya Tanzania Bara
Akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa KIPINDUPINDU nchini
Waziri Ummy Mwalimu amewasisitiza maafisa afya kuwasimamia
wajasiriamali wanaofanya biashara ya chakula na kuhakikisha wanazingatia
kanuni za afya.
0 comments:
Post a Comment