Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza
mwakani kutokana na matokeo ya darasa la saba ambapo
wanafunzi 427,60 kati ya 844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu
wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma
kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi 844,938 wamechaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983
waliofanya mtihani huo mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu
tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika
wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili
na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na
mwaka jana.
Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la
saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa
Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba
hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu
wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.
Elimu Bora Kwa Watanzania Ina Wezekana Kama Kutakuwa Na Mwamko Wa Wazazi Kwa Kuwapeleka Watoto Zao Shule.
ReplyDelete