Friday, 18 December 2015

on Leave a Comment

Tanzania:Vyombo vya Habari kuwalipa wasanii wanapopiga Nyimbo zao


Serikali ya awamu ya tano imeanza kutimiza kwa vitendo kauli ya kuifanya sanaa kuwa moja ya shughuli za kiuchumi baada ya kupitisha sheria ambayo inavitaka vyombo vya habari hapa nchini kuwalipa wanamuziki pindi wanapotumia nyimbo zao.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji CHARLES MWIJAGE amesema sheria hiyo itaanza kufanya kazi JANUARY MOJA mwaka 2016 huku waziri wa habari, utamaduni , sanaa na michezo NAPE NNAUYE akisema sasa wameanza kutekeleza yale waliyoyapanga kuyanfanya kwenye kukuza sanaa hapa nchini.

Katika kutimiza suala hilo chama cha hakimiliki hapa nchini (COSOTA) kimeingia mkataba na kampuni ya CMEA ili kuweza kufuatilia mapato ya kituo cha RADIO au TELEVISION inayopiga kazi ya mwanamuziki na kuweza kujua malipo yake yawe ya namna gani kwa mwezi.



0 comments:

Post a Comment