Thursday, 17 December 2015

on Leave a Comment

Maelfu Waandamana Kupinga Utawala wa Jacob Zuma Afika Kusini

Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma.
Wanasema visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.
Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.

Jana Bw Zuma, akiongoza sherehe za kuadhimisha Siku ya Maridhiano, ameahidi kukabiliana na ukosefu wa usawa miongoni mwa watu wa asili mbalimbali.
Hakuzungumzia maandamano dhidi yake.


0 comments:

Post a Comment