Lorraine Marriot (pichani) akiwa katika vazi la ubunifu
la Taifa .Vazi hili limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar na
imeitwa ‘Angel of Ivory’ maana inaonyesha Malaika wa Tanzania anayelinda Tembo
wanaouwawa kwa ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu.
Huyu malaika wa Tanzania yupo kwa ajili ya kuwalinda
Tembo na rasilimali zetu na kuwaadhibisha majangili. Nguo yake imeshonwa kwa
ubunifu na umahiri mkubwa na hekaheka limebuniwa na Mwanakombo Salim. Pia
kabeba fimbo la kimasai iliyonakshiwa na rangi za taifa.
Rangi nyekundu ni alama ya damu ya tembo iliyomwagika na
kusafishwa na malaika huyu.
0 comments:
Post a Comment