Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai
kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo!
Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.
Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini
wakati wa sakata la TegetaEscrow.
Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo
avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu.
Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa
hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa
kuwa Waziri?
Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi
inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye
sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu.
Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena
makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni
ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha
TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata
mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa
udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa
Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria
Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye
akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye
ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo
By: Zitto Kabwe
0 comments:
Post a Comment