Friday, 18 December 2015

on Leave a Comment

Video:Bomoa Bomoa Dar es Salaam Disemba 17 Sio Mchezo!!


17 Dec 2015 kazi ya kuwahamisha wananchi wote waishiyo katika maeneo hatarishi iliendelea kwa kuzibomoa nyumba zote zilizopo mabondeni katika baadhi ya maeneo Dar es salaam ikiwa ni pamoja na bonde la Msimbazi lililopo Kinondoni, 

tazama hii video kujionea mwenyewe

Continue Reading here...
on Leave a Comment

Washitakiwa TRA Waachiwa kwa Dhamana


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es salaam yawaachia kwa dhamana ya shilingi bilioni 2 .1 washitakiwa 3 kati ya 8 wanaotuhumiwa kwa makosa ya hujuma katika ukusanyaji mapato TRA.

Continue Reading here...
on 1 comment

Serikali Yatangaza Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2016


Serikali imetangaza watakaoingia kidato cha kwanza  mwakani  kutokana na matokeo ya darasa la saba  ambapo wanafunzi  427,60 kati ya  844,938 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu ikiwa ni asilimi 50.61 huku ikisisitiza hakuna asiyejua kusoma kuhesabu na kuandika .
Jumla ya wanafunzi  844,938 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika shule za serikali kati ya wanafunzi 867,983 waliofanya mtihani huo mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Bw. Jumanne Sagini amesema katika wanafunzi waliofaulu 16,482 wamekosa nafasi na kwamba watasubiri chaguo la pili na kwamba katika mitihani hiyo vitendo vya udanganyifu vilipungua tofauti na mwaka jana.

Kuhusu kuwepo kwa wanafunzi ambao wamemaliza darasa la saba mwaka huu huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika katibu mkuu huyo wa Tamisemi amesema hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyemaliza darasa hilo la saba hakiwa hajui kusoma na kuandika na kwamba hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema sekta ya elimu hapa nchini.



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Lorraine Marriot Miss Universe Tanzania 2015 ndani ya Las Vegas na Vazi la Taifa


Lorraine Marriot (pichani) akiwa katika vazi la ubunifu la Taifa .Vazi hili limebuniwa na Adam Hassana Kijangwa kutoka Zanzibar na imeitwa ‘Angel of Ivory’ maana inaonyesha Malaika wa Tanzania anayelinda Tembo wanaouwawa kwa ujangili kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu.

Huyu malaika wa Tanzania yupo kwa ajili ya kuwalinda Tembo na rasilimali zetu na kuwaadhibisha majangili. Nguo yake imeshonwa kwa ubunifu na umahiri mkubwa na hekaheka limebuniwa na Mwanakombo Salim. Pia kabeba fimbo la kimasai iliyonakshiwa na rangi za taifa.

Rangi nyekundu ni alama ya damu ya tembo iliyomwagika na kusafishwa na malaika huyu.


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Newspapers Headlines in Kenya 18 December





Continue Reading here...
on Leave a Comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Disemba 18











Continue Reading here...
on Leave a Comment

Tanzania:Vyombo vya Habari kuwalipa wasanii wanapopiga Nyimbo zao


Serikali ya awamu ya tano imeanza kutimiza kwa vitendo kauli ya kuifanya sanaa kuwa moja ya shughuli za kiuchumi baada ya kupitisha sheria ambayo inavitaka vyombo vya habari hapa nchini kuwalipa wanamuziki pindi wanapotumia nyimbo zao.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji CHARLES MWIJAGE amesema sheria hiyo itaanza kufanya kazi JANUARY MOJA mwaka 2016 huku waziri wa habari, utamaduni , sanaa na michezo NAPE NNAUYE akisema sasa wameanza kutekeleza yale waliyoyapanga kuyanfanya kwenye kukuza sanaa hapa nchini.

Katika kutimiza suala hilo chama cha hakimiliki hapa nchini (COSOTA) kimeingia mkataba na kampuni ya CMEA ili kuweza kufuatilia mapato ya kituo cha RADIO au TELEVISION inayopiga kazi ya mwanamuziki na kuweza kujua malipo yake yawe ya namna gani kwa mwezi.



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Spika wa Bunge Job Ndugai Yupo India kwa Matibabu.


Spika wa Bunge, Job Ndugai ni mgonjwa na yupo India kwa matibabu.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa Ndugai yuko nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake bila ya kusema amekwenda nchi gani wala ugonjwa unaomsumbua.

“Ni kweli Spika yupo nje, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi tu, siyo kwamba anaumwa sana, hapana ila hii ni mara ya pili kwenda kufanya uchunguzi huo. Hata ukitaka kuzungumza naye mpigie simu mtazungumza naye maana hali yake inaendelea vizuri na yuko salama,”alisema Dk Kashilila.

Balozi wa Tanzania nchini India, John Kijazi alipopigiwa simu ili kujua kama kiongozi huyo yuko huko, alisema:

“Ni kweli yuko hapa India kwa matibabu na anaendelea vizuri. Unaweza kumpigia wewe mwenyewe uzungumze naye.”

 Alisema Kijazi bila kuweka wazi kwamba yuko hospitali gani na nini hasa kinachomsumbua.


Continue Reading here...

Thursday, 17 December 2015

on Leave a Comment

Zitto Kabwe Aibuka na Kutetea Uteuzi wa Waziri Profesa Muhongo....Ashangaa Wanaoupinga


Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.

Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪TegetaEscrow. 

Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. 

Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?

 Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?

Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. 

Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO

2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo

By: Zitto Kabwe


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Serikali Yatoa Siku 14 Kwa Wageni Walioajiriwa Nchini Bila Kuwa na Vibali Halali


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Rais Magufuli HATANII Awafukuza Kazi Watumishi wanne wa Serikali Waliosafiri kwenda nje ya nchi bila Ruhusa


Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 17








Continue Reading here...
on Leave a Comment

Kenya Newspapers front pages 17 December 2015








Continue Reading here...
on Leave a Comment

Uuzwaji wa Matunda yaliyo Katwakatwa Wapigwa Marufuku


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amepiga marufuku biashara ya uuzaji wa  matunda yaliyokatwakatwa pamoja  na uuzaji wa chakula katika mazingira yasiyo salama ili kukabiliana na ugonjwa wa KIPINDUPINDU ambao umesambaa katika mikoa 21 ya Tanzania Bara

Akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa KIPINDUPINDU nchini Waziri  Ummy Mwalimu  amewasisitiza maafisa afya kuwasimamia wajasiriamali  wanaofanya biashara ya chakula na kuhakikisha wanazingatia kanuni za afya.



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Maelfu Waandamana Kupinga Utawala wa Jacob Zuma Afika Kusini

Maelfu ya watu wameandamana katika miji mikuu ya Afrika Kusini wakitaka kutimuliwa kwa Rais Jacob Zuma.
Wanasema visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka sana.
Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika Kusini.

Jana Bw Zuma, akiongoza sherehe za kuadhimisha Siku ya Maridhiano, ameahidi kukabiliana na ukosefu wa usawa miongoni mwa watu wa asili mbalimbali.
Hakuzungumzia maandamano dhidi yake.


Continue Reading here...

Wednesday, 16 December 2015

on Leave a Comment

Hofu ya Ugonjwa Wa Homa Ya Nguruwe Mwanza Serikali yatoa Ufafanuzi

Serikali mkoani Mwanza imewatoa hofu wananchi kuhusu ugonjwa wa homa ya nguruwe uliozuka mkoani humo kuwa haina madhara kwa watumiaji na wafugaji wa kitoweo kilichoathiriwa na ugonjwa huo

Tazama video 


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Mkurugenzi Wilaya Ya Babati Asimamishwa Kazi

Katibu mkuu TAMISEMI Mhe. Jumanne Sagini amsimamisha kazi mkurugenzi wa wilaya ya Babati kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma



Continue Reading here...
on Leave a Comment

Breaking Newzzz..Vita Juu ya Rushwa Raisi Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurungezi Mkuu wa TAKUKURU


Rais Magufuli amefanya mabadiliko Taasisi ya TAKUKURU na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,
 Dk. Edward Hoseah ambapo kamteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola kukaimu nafasi hiyo.

Taarifa kutoka Ikulu hii hapa ambapo ametangaza pia kuwasimamisha kazi watumishi wawili ambao walisafiri nje ya nchi kinyume na maagizo yake.


Continue Reading here...
on Leave a Comment

Lowassa Kuzunguka Nchi zima kuanzia Kesho


Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Ndugu Edward Lowassa atazungumza na wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tanga, siku ya Alhamis, Desemba 17, 2015.

Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama na UKAWA kwa ujumla ambao watakwenda maeneo mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na agenda nzima ya MABADILIKO katika uchaguzi mkuu uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Itakumbukwa kuwa mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na UKAWA na kuongeza nguvu kubwa ndani ya bunge hususan kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali yao mbadala huku wakiviamini vyama hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.

Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia UKAWA.

Katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na viongozi wengine waandamizi wa UKAWA ukiwa ni mwanzo tu wa ziara kubwa itakayokwenda nchi maeneo mbalimbali nchi nzima.

Imetolewa Jumanne, Desemba 15, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Continue Reading here...
on Leave a Comment

Kenya Newspapers font pages 16 December






Continue Reading here...
on Leave a Comment

Mbowe Afunguka juu ya Kasi ya Rais Magufuli.....Adai Upinzani Haimaanishi Kupinga Kila Kitu


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia kasi aliyoanza nayo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na baraza lake la mawaziri.

Akizungumza jana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Mbowe alisema kuwa rais Magufuli ameanza vizuri kiutendaji na kwamba ameanza kuzifanyia kazi hoja zilizokuwa zikihubiriwa na Chadema ndani na nje ya Bunge.

“Hoja ya kubana matumizi ya serikali, hoja ya kupunguza sherehe za kitaifa, hoja ya kupunguza safari za nchi za nje kwa viongozi wetu, hoja ya kupunguza watumishi wa umma ambao hawana umuhimu, hoja ya kuwa na serikali ndogo. Haya mambo tulizungumza siku zote na hawa hawa wa Chama cha Mapinduzi ndio waliokuwa wanayapinga haya,”alisema Mbowe.

Mbowe alieleza kuwa dhana ya upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali hivyo chama chake hakitakuwa tayari kupinga mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama baadhi ya watu wanavyotarajia, bali kitajikita katika kujadili na kuibua hoja za msingi.

“Kuwa mpinzani sio kupinga kila jambo linalofanyika hata kama likiwa jema. Sasa sisi kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na hata nje ya bunge ni wajibu wetu katika wakati wote ule kuhakikisha tunaisimamia serikali ili anachokisema rais kweli kitekelezwe kwa vitendo na isiwe hoja ya rais pekee,”alisema.

Hata hivyo, Mbowe alikosoa uteuzi wa baadhi ya mawaziri katika baraza la serikali ya awamu ya tano hususan Dk. Harison Mwakyembe ambaye wizara ya Uchukuzi aliyokua akiiongoza awali imekumbwa na sakata la upotevu wa makontena bandarini na Profesa Sospeter Muhongo ambaye amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini baada ya kujiuzulu katika nafasi hiyo wakati wa serikali ya awamu ya nne kufuatia sakata la Escrow.




Continue Reading here...
on Leave a Comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Disemba 16








Continue Reading here...